IQNA

Human Rights Watch yakosoa ukiukwaji wa haki za wafuasi wa dini na madhehebu za wachache Saudi Arabia

12:21 - November 13, 2008
Habari ID: 1707792
Jumuiya ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights Watch imekosoa vikali ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya dini zenye wafuasi wachache nchini Saudi Arabia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Human Rights Watch tawi la Mashariki ya Kati Sara Lee Whitson amesema katika ripoti ya shirika hilo kwamba katika hali ya sasa vyombo vya serikali ya Saudi Arabia vinafanya ubaguzi wenye mpangilio maalumu dhidi ya raia wa madhehebu ya Shia na dini nyingine zenye wafuasi wachache.
Taarifa hiyo ya ubaguzi wa vyombo vya serikali ya Riyadh imetolewa huku Mfalme wa nchi hiyo Abdullah bin Abdulaziz akisimamia mkutano wa "Mazungumzo Kati ya Dini Mbalimbali" mjini New York na kuwataka walimwengu kuitikia wito wa ujumbe wa amani na maelewano ya kidini! na wakati huohuo wafuasi wa madhehebu na dini za wachache nchini kwake wakinyimwa haki za kutekeleza kwa uhuru nyadhifa zao za kidini na kimadhehebu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Human Rights Watch tawi la Mashariki ya Kati Sara Whitson amewataka washiriki katika mkutano wa Mazungumzo Kati ya Dini Mbalimbali mjini New York kuishinikiza Saudi Arabia ili ikomeshe ubaguzi wa kidini na kimadhehebu. Amesema, kualikwa viongozi wa ngazi za juu wa utawala ghasibu wa Israel katika mkutano huo ulioitishwa na Saudi Arabia kunaweka wazi utambulisho na sura yake halisi.
Ripoti ya Human Rights Watch imesema: Raia Waislamu wa madhehebu ya Shia na wafuasi wa dini za waliowachache hawaruhusiwi kutekeleza faradhi zao za kidini hadharani na kwamba Waislamu wasiofuata mafundisho ya Kiwahabi wanakabiliwa na matatizo katika kutekeleza ada na desturi zao za kiibada na kidini huko Saudia.
Ripoti hiyo imeitaja inayoitwa Kamati ya Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu ya Saudi Arabia kuwa ni "polisi ya kidini" ambayo daima huwafuatilia Waislamu katika utekelezaji wa nyadhifa zao za kidini.
Ripoti za jumuiya za kutetea haki za binadamu zinaonyesha kwamba ubaguzi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaoishi katika maeneo ya mashariki mwa Saudi Arabia, unaongezeka siku baada ya siku. 319374
captcha