IQNA

Nembo ya dhahabu ya kuba na minara ya haram ya Imam Ali (as) yatunukiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

10:50 - November 15, 2008
Habari ID: 1708271
As'ad Sultan Abu Kulal, mkuu wa mkoa wa mji mtakatifu wa Najaf amemtunuku Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nembo ndogo ya dhahabu ya kuba na minara ya haram ya Imam Ali (as).
Abu Kulal alimtunuku Ban Ki Moon nembo hiyo baada ya kukutana na kuzungumza naye huko mjini New York, makao makuu ya umoja huo. Mkuu huyo wa mji wa Najaf amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa ajili ya kuifahamisha taasisi hiyo muhimu ya kimataifa thamani na shakhsia tukufu ya Imam Ali (as). As'ad Sultan Abu Kulal vilevile amehudhuria kikao maalumu kilichoandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutoa ripoti kuhusiana na safari yake katika nchi kadhaa za Asia na Afrika. Nembo hiyo ya haram ya Imam Ali (as) iliyotunukiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa itahifadhiwa daima katika makao makuu ya umoja huo. 320125
captcha