Kipindi hicho kimetayarishwa kwa lengo la kuchunguza matoleo ya magazeti, majarida na maandiko ya saiti mbalimbali za intaneti na vyombo vya habari vya ndani na nje vinavyojadili matukio ya ulimwengu wa Kishia na Kiislamu kwa ujumla. Vilevile kimejadili matukio na minasaba mbalimbali ya kidini kama kumbukumbu ya siku za kuzaliwa au kuuawa shahidi Maimamu watoharifu kutoka kizazi cha Mtume Muhammad SAW. Kipindi cha View Point cha kanali ya televisheni ya Sahar pia kimechunguza mchezo wa video unaohusiana na mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia huko Ujerumani, vitendo vya uhasama dhidi ya Waislamu katika nchi za Ulaya na kadhalika.
Kanali ya televisheni ya satalaiti ya Sahar inapatikana katika satalaiti za Asiasat 3S na Hotbird 8. 319956