Hayo yamesemwa na Muhammad Mukhtar, mwanachuo wa Kiislamu na msomaji wa Qur'ni kutoka Guenea ambaye ameshiriki katika duru ya pili ya Mashindano ya Kimataifa ya usomaji Qur'ani kwa wanchuo wa Kiislamu yaliyomalizika siku ya Ijumaa mjini Tehran. Mwanachuo huyo wa Kiislamu amesema kuwa umoja wa umma wa Kiislamu unaweza kupatikana tu kwa Waislamu kuzingatia mafundisho ya Qur'ani na kutatua matatizo yao kwa kukitegemea kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. Amesema, kama tunavyojua sote idadi ya Wakristo ni kubwa kuliko ya Waislamu ulimwengu na kusisitiza kwamba jambo hilo linafanya haja ya Waislamu kushirikiana kuwa kubwa zaidi na kwamba ili kufikia lengo hilo, Waislamu wanapasa kushikamana na kupuuza tofauti ndogondogo walizonazo. Amesema hakuna nchi yoyote inayozingatia Uislamu na kuandaa vikao na mikutano ya kimataifa ya Kiislamu kama inavyofanya Iran na kuongeza kuwa, jambo hilo linabainisha wazi nafasi muhimu ya Iran katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema kuwa kuna nchi nyingi tu duniani zinazojiita kuwa ni za Kiislamu lakini hazizingatii masuala muhimu katika Uislamu kama vile ya kuvaa hijabu wala kuharamisha ulevi, jambo linalozifanya kutofaa kujumuishwa katika kundi la nchi za Kiislamu. Muhammad Mukhtar amesifu jinsi mashindano ya duru hii yalivyofanyika na kusema kuwa, kualikwa wasomaji na marefa mushuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu katika mashindano hayo ni jambo lililo na maslahi na manufaa makubwa kwa Waislamu. Amesema wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani wanapasa kufuata mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu na kutoa mfano mzuri kwa wenzao katika jamii. 320262