IQNA

Kongamano la kielimu la “Ustawi wa Elimu ya Teolojia ya Kiislamu” nchini Russia

12:48 - November 16, 2008
Habari ID: 1708748
Kongamano la Ustawi wa Elimu ya Teolojia ya Kiislamu na Kidini nchini Russia lilianza jana katika hoteli ya Golden Ring kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Moscow na Baraza la Mamufi wa Russia.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu nchini Russia Abu Dhar Ibrahimi ambaye aliwasilisha makala katika kongamano hilo amiambia IQNA kwamba makala yake iliyokuwa na kicha cha maneno: “Mchango wa Mafunzo ya Kiislamu Katika Kutokomeza Ugaidi na Misimamo Mikali” imejadili maudhui za historia ya neno ugaidi, ugaidi na Tangazo la Kimataifa la Haki za Binadamu, udharura wa kuzuia ugaidi katika dunia ya sasa, taathira ya akhlaki na maadili mema katika kutokomeza ugaidi, na athari za mafundisho ya Kiislamu katika kukabiliana na ugaidi.
Amesema kuwa mafunzo ya dini zote zinazompwekesha Mwenyezi Mungu za Uislamu, Ukristo na Uyahudi yanasisitiza juu ya upendo, urafiki na amani na kwa maana nyingine ni kuwa, mauaji na ugaidi ni vitu vinavyopingana na dini. Amesisitiza kuwa chanzo cha ugaidi kinapaswa kutafutwa katika ukosefu wa imani ya dini na si katika imani za dini za mbinguni.
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran mjini Moscow amesema, kongano hilo lilihutubiwa na shakhsia na viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mufti na Mkuu wa Kitengo cha Dini ya Kiislamu kanda ya Ulaya wa Russia, Waziri wa Masuala ya Dini wa Uturuki, Naibu Waziri wa Elimu wa Russia, Mufti wa Tatarstan, Mshauri Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Russia, Viongozi wa ngazi za juu wa kanisa la Orthodox na balozi wa Saudi Arabia nchini Russia.
Kongamano hilo pia limehudhuiwa na mabalozi wa nchi za Kiislamu, jumuiya mbalimbali za kidini na wawakilishi wa vyuo vikuu vya Russia. 320537
captcha