IQNA

Kuanza kongamano la kimataifa la "Familia ya Kiislamu na Changamoto za Sasa" Saudi Arabia

10:43 - November 17, 2008
Habari ID: 1709129
Kongamano la kimataifa la kuchunguza matatizo na changamoto zinazozikabili familia za Kiislamu lilianza jana katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi Habari Waislamu Ahmad Abdurrahman Suyan amesema katika ufunguzi wa mkutano huo kwamba utumiaji wa kanali za televisheni za satalaiti na mitandao ya intaneti umekithiri katika zama za sasa, suala ambalo linatoa changamoto kubwa na kusababisha matatizo kwa familia za Kiislamu.
Amesema kuwa kuongezeka idadi ya talaka, vitendo vya utumiaji mabavu ndani ya familia na kupungua kwa mchango wa familia za Kiislamu katika malezi ya watoto katika nchi za kiislamu kumetayarisha uwanja wa uingiliaji kati wa jumuiya za kimataifa zikiwemo za kutetea haki za binadamu.
Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu wa Saudi Arabia Saleh Abdulaziz Al al Sheikh pia alihutubia mkutano huo akisisitiza juu ya nafasi ya maulama, walinganiaji wa dini na taasisi za mahubiri ya Kiislamu katika kuwazindua Waislamu na kuwahamasisha kufuata njia ya wastani.
Wahadhiri wa vyuo vikuu na wasomi wanaohudhuria kongamano hilo la kimataifa wamewasilisha makama mbalimbali zinazojadili maudhui ya "Changamoto Zinazoikabili Familia ya Kiislamu." 321105

captcha