Akizungumza na waandishi habari mjini Kabul, Karzai amesema kuwa, 'iwapo siku za awali za kuanza kipindi changu cha urais ningetekeleza sheria za Kiislamu nchini Afghanistan, matatizo mengi yangeweza kutatuliwa'.
Karzai ameashiria fatwa za Maulama na wasomi wa Kiislamu kuhusu kuhifadhi maadili na thamani za Kiislamu na kuzingatia sheria za kidini. 'Mara kadhaa nimekumbushwa kuwa sheria za Kiislamu zinapaswa kutekelezwa katika nchi za Kiislamu. Kutokana na mashinikizo ya kimataifa sijaweza kutekeleza sheria hizo. Lakini sasa sitawaruhusu tena wageni waingilie masuala ya ndani ya nchi', amesema Rais Hamid Karzai.
Afghanistan imekuwa katika mashinikizo ya kimataifa katika siku za hivi karibuni baada ya kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya watenda jinai nchini humo. 321366