Mkutano wa kimataifa wa Usraarabu wa Kiislamu Katika Eneo la Kusini mwa Asia” umeanza kazi zake katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka kwa ushirikiano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Bangladesh, Chuo Kikuu cha Dhaka na Kituo cha Utafiti wa Historia, Sanaa na Utamaduni wa Kiislamu cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Ajenda kuu ya mkutano huo ni kuchunguza historia na ustaarabu wa Kiislamu na mchango wa Uislamu katika vipindi mbalimbali vya historia ya eneo la kusini mwa Asia.
Kikao cha ufunguzi wa mkutano huo kimehutubiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Bangladesh Tauhid Hussein, Katibu Mtendaji wa wizara hiyo Muhammad Imran na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Historia, Sanaa na Utamaduni wa Kiislamu cha OIC Helit Erin.
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, mwakilishi wa OIC amesisitiza juu ya udharura wa kudhihirishwa historia halisi ya Uislamu, kuondoa ufahamu usiokuwa sahihi kuhusu Uislamu na kueneza hali ya maelewano na ushirikiano kati ya mataifa ya Kiislamu. 321642