Akizungumza hivi karibuni, Abdallah Alaudeen, amesema kuwa tayari makundi 59 ya shirika hilo yako tayari kutoa huduma zao kwa mahujaji kutoka katika maeneo hayo matatu. Amesisitiza kuwa tayari suhula na vifaa vinavyohitajiwa na mahujaji vimepelekwa katika maeneo ya Arafa, Jamarat, Makka na Madina. Vilevile kwa mujibu wa kauli ya Adnan Katib, mkuu wa shirika la huduma kwa mahujaji wa kusini mwa Asia, zaidi ya mahujaji nusu milioni kutoka katika nchi za eneo hilo wanatazamiwa kuhuji mwaka huu. 321565