Muhammad Khalid Masoud amesema katika sherehe za ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya "Benki na Uwekezaji wa Kiislamu" mjini Islamabad kwamba ripoti kamili kuhusu mpango wa kuoanisha sheria za sasa za Pakistan na mafundisho ya Qur'ani Tukufu na suna za Mtume SAW utawasilishwa kwa umma hivi karibuni.
Khalid masoud pia amefafanua mipango ya baadaye ya Baraza la Fikra za Kiislamu la Pakistan katika warsha hiyo.
Wakati huo huo Mshauri wa Benki za Serikali ya Pakistan Parvez Said amesisitiza juu ya udharura wa kustawishwa benki za Kiislamu si katika nchi za Kiislamu pekee bali katika nchi zote. Amesema, katika hali ya sasa zaidi ya matawi 360 ya benki ya Kiislamu yanafanya kazi nchini Pakistan.
Mshauri wa Benki za Serikali ya Pakistana amesema, uthabiti wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu katika migogoro ya kiuchumi ya kipindi cha sasa duniani umeonyesha ubora wa mfumo huo. 322228