IQNA

Onyo dhidi ya gazeti la Newsweek la Russia kwa kuwatusi Waislamu

12:39 - November 20, 2008
Habari ID: 1710463
Mwendesha Mashtaka wa Moscow Jumanne iliyopita alitoa onyo dhidi ya gazeti la Newsweek linalochapishwa mjini humo kwa kukiuka sheria za magazeti na kuchapisha makala ambazo zinatusi na kuwadharau Waislamu.
Mwezi Oktoba uliopita, gazeti hilo lilichapisha makala mbili ambazo zilitusi na kuwakosea heshima Waislamu. Vilevile moja ya vikatuni vilivyochapishwa na magazeti ya Denmark na kuzusha maandamano na malalamiko makubwa ya Waislamu ulimwenguni pia kilichapishwa katika gazeti hilo hivi karibuni. Gazeti hilo linalochapishwa nchini Russia ni sawa kabisa na lile linalochapishiwa nchini Marekani lakini likiwa na tofauti hii kwamba gazeti linalochpishiwa mjini Moscow linachapishwa kwa lugha ya Kirusi na makala zake nyingi zinahusiana na siasa za serikali ya Russia. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Russia ina Waislamu wapatao milioni ishirini. 322779
captcha