IQNA

Kuimarishwa ofisi za huduma za utalii unaohusiana na hija nchini Ufaransa

12:37 - November 20, 2008
Habari ID: 1710465
Mawaziri wa Mambo ya Ndani, Nje na Uchumi wa Ufaransa wametaka ofisi zote za kutoa huduma za utalii unaohusiana na hija kupewa nyaraka na vibali rasmi kwa ajili ya kulinda na kudhamini haki za mahujaji wanaozuru Makka.
Amesema, kwa mujibu wa makaratasi ya utangazaji yaliyotochapishwa na wizara hizo, ofisi hizo za huduma za safari za hija zinahitajika kuwapa mahujaji habari kamili kuhusiana na viza, mikataba ya safari hizo, bima na radiamali ya mahujaji kuhusiana na safari wanazofanya katika ardhi takatifu ya Makka. Amesema, ofisi hizo pia zinatakiwa kutoa habari na maelezo zaidi kuhusiana maelekezo ya mahujaji wanaonuia kuzuru maeneo matakatifu katika ardhi hiyo. Ofisi hizo zinatakiwa kupata vibali rasmi kutoka kwa serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kuendesha shughuli za kutoa huduma za hija na wakati huohuo kukubali kudhamini haki zote zinazohusiana na mahujaji. Mahujaji wowote watakaohisi kuwa wamedhulumiwa au kupuuzwa haki zao kuhusiana na suala hilo watatakiwa kuvijulisha vyombo husika vya serikali ili kulifuatilia. 322777
captcha