Duru ya 32 ya Tamasha la Kimataifa la Filamu la Cairo limeanza rasmi kwa kuhudhuriwa na Farouq Hassani, Waziri wa Utamaduni wa Misri, na kwa kuongezwa nyanja nyingine mpya ya 'Usamehevu wa Uislamu katika Ulimwengu wa Sinema' katika tamasha hilo.
Filamu saba tayari zimewasilishwa katika nyanja hiyo. 'Waislamu' kwa uongozi wa Iddris Bur Amul, mwongozaji filamu wa Kimarekani, ni moja ya filamu ambazo zimewasilishwa katika nyanja hiyo. Madhumuni ya filamu hiyo ni jinsi vyombo vya habari vya Marekani vinavyopotosha sura halisi ya Uislamu katika kuiarifisha dini hii tukufu. Inakumbushwa hapa kuwa, filamu 150 zikiwemo tisa za Misri, zitaonyeshwa katika tamasha hilo litakalozishirikisha nchi 59. 323007