IQNA

Uwezo wa Afrika katika kuwekeza kwenye mfumo wa Benki ya Kiislamu

11:10 - November 22, 2008
Habari ID: 1710987
Katika miaka kumi ya hivi karibuni mfumo wa Benki ya Kiislamu umestawi kwa asilimia 20 kwa kuwa na rasilimali ya kati ya dola bilioni 500 hadi 700 mbazo zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Hata hivyo hisa ya bara la Afrika katika rasilimali hiyo ni ndogo mno licha ya bara hilo kuwa na zaidi ya jamii ya Waislamu milioni 412 yaani yapata nusu ya wakazi wote milioni 850 wa Afrika.
IQNA imenukuu Webmanagercenter kwamba taarifa ya mwisho ya kongamano la siku mbili lililofanyika mapema mwaka huu mjini Dakar, Senegal, ilisisitiza kuwa kwa kuzingatia ukubwa wa jamii ya Waislamu barani Afrika, udhaifu sugu wa kiuchumi wa bara hilo unapaswa kuondolewa kwa kutegemea sheria za Kiislamu. Taarifa hiyo ilisema kuwa mfumo wa benki ya Kiislamu unatumiwa katika benki chache mno barani Afrika licha ya kupokelewa kwa wingi na kwamba badhi ya wataalamu wanaona kuwa nchi za Afrika zinaweza kutumia fursa ya kuwekeza katika sekta za maskani, magari na kadhalika.
Kwa mujibu wa shirika la uwekezaji la Moody’s Investors Services, uwezo wa kifedha na Kiislamu wa bara Afrika unaweza kuongezeka hadi dola bilioni 230. Shirika hilo limesema kuwa mfumo wa Benki ya Kiislamu ni njia bora zaidi kwa nchi huru zinazotaka kutumia mfumo wa Kiislamu katika kuimarisha uchumi wao. 321722
captcha