Shirika la Elimu, Utamaduni na Sayansi ya Kiislamu ISESCO litashiriki katika kikao cha Mawaziri wa Utamaduni wa Baraza la Ulaya kilichopangwa kufanyika tarehe pili na tatu mwezi Disemba katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku.
Habari kutoka ISESCO zinasema kuwa kikao hicho kitakachosimamiwa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya Azerbaijan na Baraza la Ulaya kitahudhuriwa pia na Mawaziri wa Utamaduni wa nchi kadhaa wanachama wa ISESCO kama Jordan, Imarati, Qazakhstan, Saudi Arabia, Turkmenistan, Tajikistan, Misri, Libya, Morocco, Qatar, Malaysia, Senegal na Tunisia.
Washiriki watajadili madhui ya uchunguzi huru kuhusu mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali, thamani za kimataifa katika tamaduni za kijadi, siasa na sera za kiutamaduni, urithi wa kiutamaduni na uhusiano wake na mazungumzo kati ya tamaduni na kadhalika. 323427