IQNA

Hujuma ya utamaduni wa kigeni Afghanistan yazidi

12:24 - November 22, 2008
Habari ID: 1711048
Viongozi wa ngazi za juu wa kidini, kitamaduni na kisiasa nchini Afghanistan wameikosoa serikali kwa kutojali kuhusu hujuma ya kitamaduni inayofanyika nchini humo na kuwafanya Waafghani kuwa mbali na mafunzo ya dini ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA huko Afghanistan, Hujatul-Islam Sayyid Hakim Shah mmoja kati ya maulamaa wa mkoa wa Faryab, amesema, ni jambo lisilokubalika kwa serikali ya Afghanistan kupuuza na kuhimiza utangazaji wa filamu za Kihindi katika televisheni ya nchi hiyo. Amesema, filamu hizo zinawapoteza vijana na kuchochea vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya watoto.
Ameongeza kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua dhidi ya upotofu wa kitamaduni na kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanapata muongozo bora kuelekea saada na maadili mema.
Abdulwahab Kuhi Wakili wa watu wa mkoa wa Faryab anayewakilisha mitaa 9 ya mji wa Madimne katikati mwa mkoa huo vile vile ameikosoa serikali kwa kutozingatia hali ya maisha ya watoto. Amesema, hivi sasa nchini Afghanistan kuna watoto millioni moja wasio na wazazi katika hali ambayo hakuna bajeti yoyote iliyotengwa kwa ajili ya watoto hao.
Kuhusiana na hilo Mohammad Is-haq mmoja wa waalimu wa Faryab amekosoa namna wazazi na waalimu shuleni wanavyodhoofisha motisha miongoni mwa watoto. Amesema, 'jamii inapaswa kutunukiwa mtoto mwenye motisha wa juu na ujasiri wa kutosha'. Naye Dhabihullah Peyman Mkuu wa Idara ya Haki za Binaadamu katika mkoa wa Faryab amelaani utumiaji nguvu na mabavu dhidi ya watoto wa Afghanstan hasa katika mkoa huo na kuvitaka vyombo vya mahakama kuchukua hatua kali dhidi ya wanaohujumu haki za watoto.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Faryab Abdulhaq Shafiq amesema, Uislamu ni dini ya wastani na kwamba Waislamu hawapasi kunyamazia kimya utumiaji mabavu na ukatili. Ameongeza kuwa, katika kipindi chote cha maisha yao, watoto wanahitajia kuzingatiwa kikamilifu ili waweze kukua vizuri na kuifaidisha jamii.
323282
captcha