IQNA

Kikao cha ‘Fikra ya Imam Hussein (as) na Taathira zake kwa Fasihi ya Iraq’ chafanyika Karbala

8:26 - November 24, 2008
Habari ID: 1711714
Kikao cha kitaifa cha kuchunguza taathira za mapambano na fikra ya Imam Hussein (as) kwa fasihi ya Iraq kimefanyika katika mji mtakatifu wa Karbala.
Kikao hicho kiliandaliwa na Taasisi ya Sayyidu Shuhadaa ya Karbala ambapo idadi kubwa ya wahadhiri, waandishi na wanafikra wa Kiislamu walishiriki.
Abud Judi al-Hilli, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Karbala na Muhammad Abdul Hussein al-Khatib, mmoja wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya nchini Iraq walihutubia kikao hicho ambapo waligusia nafasi na athari ya mapambano ya Abu Abdillah al-Hussein (as) katika fasihi na mashairi ya Kiarabu na hasa ya washairi wa Iraq.
Ridhaa al-Khafaji, mshairi na mwandishi wa michezo ya kuigiza wa Iraq pia alitoa hutuba katika kikao hicho ambapo alisema kwamba, fikra ya Imam Hussein (as) katika mapambano ya Karbala ilikuwa na athari ya moja kwa moja na ya kudumu milele kwa mashairi ya Wairaqi, na hasa kwa washairi na wanafasihi wa Karbala. Amesema, fikra ya Imam Hussin (as) ni fikra kamilifu kwa ajili ya kudhamini mahitaji yote ya maisha ya mwanadamu katika ulimwengu wa leo.
Inakumbushwa hapa kuwa washairi kama vile Sayyid Haidar, Sayyid Jawad Shubbar, Sayyid Ridha al-Hindi na Sheikh Muhsin Abil Hubb al-Kabir ni miongoni mwa vinara mashuhuri wa fasihi ya Imam Hussein nchini Iraq. 324341
captcha