IQNA

Kiongozi wa msafara wa Hija wa Misri atembelea ofisi ya msafara wa Hija wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Madina

14:43 - November 24, 2008
Habari ID: 1712103
Kiongozi wa msafara wa Hija wa Misri Brigedia Jenerali Muhammad al Masri amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa msafara wa Hija wa Iran katika ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Madina.
Katika mazungumzo hayo Brigedia Jenerali Muhammad al Masri ameashiria utamaduni wa siku nyingi, ustaarabu na masuala mengi yanayozikutanisha tamaduni za Misri na Iran na akasisitiza juu ya udharura wa viongozi wa Cairo na Tehran kuondoa hitilafu za pande mbili na kujenga uhusiano madhubuti katika nyanja mbalimbali.
Al Masri ameeleza kuridhishwa na mazungumzo yake na viongozi wa misafara ya Hija na akaelezea matumaini ya kukutana na kiongozi wa msafara wa Hija wa Jamahuri ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Muhammad Muhammadi Reyshahri katika siku chache zijazo.
Katika mazungumzo ya pande hizo mbili ilikumbushwa kwamba mbegu za wa awali za kuimarisha umoja kati ya makundi mbalimbali ya Kiislamu katika zama za sasa zilipandwa nchini Iran na Misri katika zama za Sheikh Shaltut na kusisitiza kwamba uhusiano na mashirikiano zaidi kati ya nchi hizo mbili yataunufaisha ulimwengu mzima wa Kiislamu. 324375

captcha