Kwa mujibu wa gazeti la Peninsula, katika duka hilo kuna vitabu vinavyohusu usanifu majengo wa Kiislamu, fasisi, mashairi na utamaduni wa Kiislamu.
Vitabu vya marejeo na muongozo wa Jumba la Makumbusho ya Kiislamu mjini Doha pia vinauzwa katika duka hilo.
Jumba la Makumbuso la Sanaa za Kiislamu nchini Qatar limefunguliwa hivi karibuni katika sherehe zilizohudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbali mbali duniani. Jumba hilo la makumbusho lina ghorofa tano. Kituo hicho cha utamaduini kina vifaa 1000 vya sanaa kutoka zama mbali mbali za ustaarabu wa Kiislamu.
325146