Talal bin Ahmad Aqil amesema kuwa mpango huo wa kugawa Qur’ani kwa mahujaji unasimamiwa na Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia na kwamba karibu kanda za sauti milioni tatu zinazofafanua jinsi ya kutekeleza amali za Hija zitatolewa kwa mahujaji.
Amesisitiza kwamba shughuli ya upashaji habari na maelezo kwa mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu mwaka huu kuhusu utekelezaji wa amali za Hija inafanyika kwa kiwango cha juu.
Talal Ahmad Aqil amesema, zimewekwa televisheni kubwa kwenye medani za miji ya Makka na Madina mbazo zinaonyesha picha zinazotoa maelezo kuhusu amali za Hija na kwamba vyombo mbalimbali vya habari vya Saudia vinarusha hewani vipindi tofauti kuhusu utekelezaji wa ibada hiyo.
Msimamizi wa Kamati ya Maelezo na Upashaji Habari ya Saudi Arabia amesema kuwa Wizara ya Waqfu ya nchi hiyo inashirikiana pia na karibu televisheni 40 za satalaiti katika kupasha habari na kutoa maelezo kwa mahujaji. 325043