Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa, wawakilishi wa jumuiya mbili hizi za kidini wametia saini mkataba ambao unawajibisha pande mbili kushirikiana kwa ajili ya kutatua matatizo yao na kupambana na mitazamo ya kidini ya kupindukia mipaka. Vilevile pande mbili hizo za kidini zimesisitiza umuhimu wa kupambana na makundi yanayoeneza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Ufaransa. Wawakilishi wa dini mbili hizo za mbinguni vilevile wamesisitiza umuhimu wa kuunda kundi litakalowakisha wawakilishi wa pande hizo ili kutetea haki za wafuasi wa dini za mbinguni na vilevile haja ya kufundisha vijana masuala muhimu yanayowahusu na vilevile dini zao. 325566