IQNA

Kituo cha kuhifadhi na kusoma Qur’ani kufunguliwa nchini Nigeria

11:26 - November 26, 2008
Habari ID: 1712905
Wakuu wa jimbo la Zamfara kaskazini magharibi mwa Nigeria wameazimia kuanzisha katika jimbo hilo kituo cha kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu ili kuwavutia walio na hamu ya kujifunza nyanja hizo.
Kwa mujibu wa gazeti la Nigeria la Triumph kituo hicho kimeanzishwa kwa pendekezo la Kamati ya Kuhifadhi na Kusoma Qur’ani ya Jimbo la Zamfara kwa ajili ya kuandaa uwanja wa vijana walio na vipawa kukukiza vipawa hivyo na vilevile kuwawezesha kushiriki katika mashindano ya kieneo kitaifa na kimataifa. Al-Haj Ahmad Abdullahi Gano, Katibu Mkuu wa kamati hiyo amesema kuwa, kamati hiyo imetoa pendekezo la kuanzishwa kituo hicho ikiwa ni katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria. Kamati hiyo imesema kuwa, wanafunzi watakaopewa masomo katika kituo hicho watashiriki katika mashindano mbalimbali ya kieneo na kimataifa ya Qur’ani na kupata mafanikio makubwa katika uwanja huo.
Kuratibiwa duru za masomo, kuandaa semina na warsha mbalimbali za mafunzo kwa shule za Kiislamu na kueneza utamaduni wa kuhifadhi na kusoma Qur’ani katika skuli za Qur’ani ni miongoni mwa malengo ya kamati hiyo. 325540
captcha