IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani na Hadithi nchini Qatar wapongezwa

10:57 - November 27, 2008
Habari ID: 1713214
Sherehe za kuwashukuru na kuwapongeza vijana walioshinda katika duru ya 21 ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Takatifu na Hadithi kwa Vijana wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, yalifanyika siku ya Jumatano huko katika mji wa Doha Qatar.
Mashindano hayo yalifanyika katika makundi mawili ya vijana wa kike na kiume wenye umri wa miaka 15 hadi 25 na 10 hadi 14. Vijana hao wote pia walitakiwa kuhifadhi hadithi 37 kutoka kitabu cha Riyadh al-Swaliheen cha Muhadith Nawawi. Katika kundi la umri wa 15 hadi 25 Muhammad Qassim al-Qahtani kutoka Qatar, Naif Muhammad Salim kutoka Saudi Arabia na Muhammad Ahmad al Mad'hush kutoka Oman walifanikiwa kushinda nafasi za kwanza hadi tatu kwa utaratibu, ambapo walitunukiwa nishani za dhahabu, fedha na shaba.
Katika sherehe hizo, Khalid Yusuf al-Malla, Mkuu wa Idara Kuu ya Masuala ya Vijana nchini Qatar ambaye pia alikuwa katibu wa mashindano hayo, Khalid al-Yaish, mwakilishi wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, Hamad bin Abdul Aziz al-Kuwari, Waziri wa Masuala ya Utamaduni wa Qatar na msimamizi wa Kamati ya Marefa ya mashindano hayo pamoja na shakhisa wengine wa kisiasa na kiutamaduni na vilevile wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani Takatifu kutoka sehemu mbalimbali pia walishiriki katika sherehe hizo. 326111
captcha