IQNA

Ushujaa na kujitolea kwa Masahaba wa Mtume SAW kwachunguzwa Jiddah, Saudi Arabia

11:51 - November 27, 2008
Habari ID: 1713239
Mwandishi, mtafiti na mwanafikra wa Kiislamu Abdulsattar Khan amehutubia kikao kilichofanyika mjini Jiddah akieleza ushujaa na kujitoa muhanga kwa Masahaba wa bwana Mtume Muhammad SAW.
Gazeti la Arab News limeandika kuwa mfululizo wa hotuba hizo ambazo hutolewa kila mwezi utajadili sira za Masahaba kumi wa Mtume Muhammad SAW.
Abdulmatin Othman ambaye ni mmoja wa waratibu wa hotuba hizo amesema kuwa ushujaa na ujasiri wa Masahaba kumi wa Mtume unaweza kuwa ilhamu kwa Waislamu kote duniani na kwamba mahatibu wa vikao hivyo wana ujuzi mkubwa na maarifa kuhusu Masahaba wa Mtume Muhammad SAW. 326278

captcha