Warsha ya Sanaa ya Kiislamu katika Tamaduni tofauti imefanyika mjini Doha, Qatar kwa lengo ya kuchunguza utajiri wa sanaa ya Kiislamu. Warsha hiyo imefanyika sambamba na maonyesho ya kwanza ya muda ya Jumba la Makumbusho la Sanaa ya Kiislamu la Doha.
Warsha hiyo iliyohudhuriwa na wahakiki na wataalamu wa historia kutoka nchi mbalimbali, ilichunguza utajiri wa sanaa ya Kiislamu bila ya kutilia maanani mipaka ya kijografia, tamaduni na kaumu mbalimbali.
Lengo la warsha hiyo ni kuchunguza maingiliano ya kielimu, kitamaduni na kisanii kati ya ulimwengu wa Kiislamu na tamaduni nyingine.
Warsha hiyo ilikuwa na sehemu tatu ambazo ni Uislamu na dini nyinginezo duniani, Uislamu na mabadilishano ya sanaa na Uislamu na mabadilishano ya habari. 326305