Filamu hiyo imepangwa kuonyeshwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.
Gazeti la al Jaridatul Uula la Morocco limeashiria wasiwasi wa Waislamu wa Ulaya kuhusu filamu hiyo na kuandika kwamba: Jumuiya za Kiislamu za Ulaya zimeanza kutayarisha rasimu inayohimiza kususiwa bidhaa za Uholanzi kama hatua ya kulalamikia filamu hiyo na kuzuia kuonyeshwa kwake hadharani.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Ihsan Jami mwenye umri wa miaka 23 aliwahi kutayarisha katuni chafu aliyoipa jina la ‘Maisha ya Muhammad’ ambayo inazungumzia ndoa ya Nabii Muhammad (SAW) na Bibi Aisha. Filamu hiyo ilipangwa kuonyeshwa mwezi Aprili mwaka uliopita lakini Wizara ya Sheria ya Uholanzi ilizuiya kitendo hicho. 326965