IQNA

Kongamano la "Vijana na Haki za Binaadamu kwa Mtazamo wa Imam Khomeini" lafanyika Zambia

11:42 - November 30, 2008
Habari ID: 1714058
Kongamano la "Vijana na Haki za Binaadamu kwa Mtazamo wa Imam Khomeini" lafanyika Zambia kwa lengo la kuwaelimisha wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusu mafundisho ya Qur'ani.
Kongamano hilo limefanyika kwa ushirikiano wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Lusaka, Kituo cha Ahlul Bayt na Baraza la Mji wa Livingstone.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kogamano hilo limehudhuriwa na washiriki 150 wanaojumuisha waalimu wa shule za serikali, chuo cha kutoa mafunzo kwa waalimu na kundi la viongozi wa Kikatoliki na Kiprotestanti katika mji wa Livingstone.
Washiriki wamejifunza mengi kuhusu mafunzo ya Uislamu na fikra za Imam Khomeini kuhusu haki za binaadamu na amani duniani.
Kongamano hilo lilikuwa na kamisheni tatu za 'Haki za Binaadamu, Vijana na Elimu', 'Amani katika Uislamu na Mtazamo wa Uislamu Kuhusu Ugaidi' na 'Mtazamo wa Uislamu kuhusu Familia'. 327475
captcha