IQNA

Wasanii Wairani kuonyesha "Asmaul Husna" mjini Istanbul

12:00 - November 30, 2008
Habari ID: 1714098
Maonyesho ya hati za kaligrafia ya Majina Matukufu ya Mwenyezi Mungu yaani "Asmaul Husna" yanaanza Jumatatu Desemba Mosi mjini Istanbul na kuendelea kwa muda wa siku 10.
Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamadauni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Istanbul Uturuki, maonyesho hayo yanafanyika kwa munasaba wa sikukuu ya Iddul Adha.
Mohammad Sadeqizadeh amesema, maonyesho hayo ya Asmaul Husna yanafanyika kwa ushirikiano wa Idara ya Utamdauni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Istanbul, Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kisasa la Iran na Idara ya Utamaduni ya Baraza la Mji wa Istanbul.
Ameongeza kuwa maonyesho hayo yatakuwa na zaidi ya athari 70 na bora zaidi za wanakaligrafia Waiirani.
Sadeqizadeh amesema kuwa waandishi wa hati za Quran na Hadithi za Mtume SAW nchini Uturufki wanaheshimiwa sana kutokana na kuwa sanaa hiyo inahesabiwa kuwa kazi tukufu. 327442

captcha