IQNA

Udharura wa kubuniwa jumuiya ya kimataifa ya wanachuo kwa ajili ya Wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu

11:43 - November 30, 2008
Habari ID: 1714108
Wanachuo na wasomi wa ulimwengu wa Kiislamu wanapasa kupanga mipango ya kubuni muungano wa vyuo vikuu vya Kiislamu, umoja ambao utasimamia shughuli za vyuo hivyo vyote.
Jambo hilo limesisitizwa na Shamsudeen Turkan, mkuu wa Jumuiya ya Uhusiano wa Kiutamaduni na Kidini ya Vijana na Wanachuo wa Uturuki. Akizungumza na shirika la habarila IQNA, Bwana Turkan amesema kuwa jambo hilo lina umuhimu mkubwa na kwamba linaweza kufikiwa tu kwa kupangwa ratiba yenye malengo ya muda mrefu. Hata hivyo, amesema kuwa ili kufikiwa lengo hilo, nchi zote za Kiislamu zinapasa kushirikiana. Katika upande wa pili, Bwana Turkan amezungumzia umuhimu wa kuanzishwa shirika la habari la wanachuo wa Kiislamu na kuongeza kuwa, umuhimu huo unatokana na ukweli kuwa hii leo vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuunganisha na kuanzisha mawasiliano kati ya watu, ametolea dalili Mayahudi na Wazayuni ambao amesema kuwa walitabua umuhimu wa jambo hilo mapema na kwamba hii leo wanaudhibiti ulimwengu kutokana na kudhibiti kwao vyombo vya habari. Amesema, Wazayuni wanaweza kuudhibiti fikra za waliowengi duniani na kuzielekeza watakako kupitia vyombo muhimu vya habari wanavyovidhibiti ulimwenguni. Turkan amezungumzia umuhimu wa vijana na wasomi wa Kiislamu kufanya juhudi za kuwaunganisha Waislamu na kuongeza kuwa, kuufahamu vyema Uislamu, kujua lugha kadhaa kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kati ya mataifa mbalimbali na uanachama katika jumuiya mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya Kiislamu, ni baadhi ya njia ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano kati ya Waislamu. Amesikitishwa sana na hali ya kuwa licha ya kuwa na jumuiya inayoziunganisha nchi 57 za Kiislamu, lakini nchi hizo zina uhusiano mdogo sana na hata mara nyingine kuwa na uadui mkubwa kutokana na masuala ya kisiasa na kutouelewa vyema Uislamu. Ameashiria watu kama vile Bilal wa Uhabeshi, Suheil wa Roma na Salman Farisi wa Uajemi ambao pamoja na kuwa walitoka katika mataifa mbalimbali lakini wote walikuwa pembeni ya Mtume Mtukufu (saw) na kuushughulikia Uislamu kwa moyo mkunjufu bila ya kuwa na ubaguzi wa kikabila wala kitaifa. 327217
captcha