Shirika rasmi la Habari la Syria SANA limetangaza kwamba ingawa ofisi ya Waziri Mkuu ilikuwa imetangaza likizo kuanzia Jumapili tarehe 7 Desemba hadi tarehe 11, wananchi waliowengi wametaka likizo rasmi iongezwe na kuwa siku tisa.
Watu na serikali ya Syria sawia na nchi nyinginezo za Kiarabu huzipa umuhimu mkubwa sikukuu za Idul Fitr na Idul Adh-ha. Siku kadhaa kabla ya sikukuu hizo watu wengi hununua nguo mpya kama mojawapo wa njia za kusherehekea sikukuu hizo za Kiislamu. Kutokana na jamaa na marafiki kutembeleana katika sikuukuu hizo mbili, serikali ya Syria kwa kawaida huongeza idadi ya siku za likizo ili wananchi waweza kupata muda wa kutosha kutekeleza suna hiyo muhimu. 328472