IQNA

Maonyesho ya kazi za wasanii wa Pakistan kuhusu Qur’ani Tukufu

9:57 - December 02, 2008
Habari ID: 1714887
Maonyesho ya kazi za kisanii kuhusu Qur’ani Tukufu yalianza jana mjini Islamabad katika Jumba la Sanaa la Taifa la Pakistan.
Maonyesho hayo yanajumuisha kazi 330 za kaligrafia ya Qur’ani (sanaa ya kuandika vizuri hati za Qur’ani) uandishi wa magazeti na uchoraji wa mwanafikra na mwanasiasa wa zamani wa Pakistan Muhammad Hanif Ramay. Vipande 99 vya maonyesho hayo ya kaligrafia vimepambwa kwa jina la “Allah” na “Muhammad saw” na vilichorwa na msanii Ramay kwa njia ya kipekee ili kuakisi thamani za kiroho za Uislamu.
Maonyesho hayo ambayo yataendelea hadi tarehe 19 mwezi huu wa Disemba, yanafanyika kukumbuka msanii huyo hodari wa Pakistan.
Msanii mashuhuri wa sasa wa Pakistan Rashid Bat ambaye ametembelea maonyesho hayo ya kaligrafia ya Qur’ani amesema, Ramay alikuwa kinara wa sanaa hiyo na kwamba alikuwa mtu wa kwanza kutumia mbinu mpya za kisanii katika sanaa ya kuandika vizuri hati za Qur’ani Tukufu. 328400


captcha