Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Kyrgyzstan, madrasa hiyo iitwayo “Darul Qur'ani” iliyo katika kitongoji cha mji mkuu wa Jamhuri ya Kyrgyzstan, Bishkent, imewavutia wanafunzi wengi kutokana na masomo yake ya hali ya juu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna zaidi ya wanafunzi 90 wanaosoma Qur'ani katika chuo hicho.
Mbali na kutoa mafunzo ya Qur'ani, waalimu katika chuo hicho wanafunza pia masomo mengine ya Kiislamu na wanasisitiza juu ya wanafunzi kuhudhuria masomo yote bila kufeli.
Masomo katika Madrassa ya Darul Quran kijijini Alexandar Afka hufanyika siku sita kwa wiki.
328535