IQNA

Afisa wa Hizbullah: Kuuawa shahidi Imam Khamenei kumeimarisha nguvu ya Muqawama

20:47 - July 05, 2026
Habari ID: 3482444
Mahmoud Qamati
IQNA – Naibu Mkuu wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa kuuawa Shahidi Ayatullah Seyyed Ali Khamenei kumeongeza mara mbili nguvu ya makundi ya Muqawama wa Kiislamu na watu huru duniani kote.

Akizungumza na IQNA pembezoni mwa shughuli za mazishi na kuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu jijini Tehran, Mahmoud Qamati amesema kuwa shahada hii imeupa uhai mpya mhimili wa Muqawama, na hasa kwa taifa la Iran, na kuimarisha mshikamano na umoja dhidi ya njama za maadui. “Ukweli ni kwamba Shahidi Ayatullah Khamenei alikuwa akizingatia sana mhimili wa Muqawama na hakupungua katika kuusaidia mstari huo wa mapambano. Aliyaunga mkono makundi yote ya Muqawama katika ukanda huu kwa nguvu zake zote na kwa nyenzo zote zilizokuwa mikononi mwake.” Kuhusu sababu iliyomfanya Kiongozi Shahidi kuiunga mkono kadhia ya Palestina na Quds (Jerusalem), alibainisha moja ya majukumu makuu ya mhimili wa Muqawama na kufafanua: “Palestina ndiyo dira ya ulimwengu wa Kiarabu na wa Kiislamu.

Kwa sababu hiyo, tangu wakati wa kwanza kabisa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (RA) alisisitiza umuhimu wa Palestina. Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi naye alikuwa na mtazamo huo huo na alitoa umakini na kipaumbele cha pekee kwa Palestina hadi alipouawa shahidi kwa ajili ya kadhia ya Palestina, haki, na uadilifu.” Qamati pia alifafanua sababu kuu zilizozuia mhimili wa Muqawama kushindwa mbele ya shinikizo na njama za maadui. Moja ya sababu muhimu zaidi za nguvu ya mhimili wa Muqawama ni kwamba mhimili huu uko upande wa ukweli, unaunga mkono haki, na unasimama dhidi ya batili, dhulma, na uistikbari wa kimataifa, alisema. 

“Wakati imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiyo msingi wa Muqawama na uthabiti, umoja wa nyanja mbalimbali za mapambano pia umeupa mhimili huu nguvu ya ajabu ya kukabiliana na dhulma.” Alipoulizwa kuhusu msisitizo wa Kiongozi Shahidi juu ya umoja miongoni mwa nchi za Kiislamu na kujikusanya karibu na mhimili wa Muqawama, alibainisha kuwa umoja ni nyenzo ya nguvu, kama ambavyo Imam Khomeini (RA) naye alisisitiza umoja miongoni mwa Waislamu.

“Umoja miongoni mwa nchi za Kiarabu na Kiislamu huleta nguvu, na kwa sababu hiyo, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi alisisitiza sana umoja wa Kiislamu.” Afisa huyo wa Hizbullah alizungumzia zaidi mitazamo ya Kiongozi Shahidi kuhusu dini na madhehebu: “Kama ambavyo Kiongozi Shahidi alisisitiza umoja miongoni mwa nchi za Kiarabu na Kiislamu, alikuwa pia na mtazamo mpana kuhusu dini na madhehebu mengi, akitutaka tujikomboe kutoka katika mifumo finyu tuliyozungukwa nayo na tushikamane na haki na uadilifu.” 

3498096

Habari zinazohusiana
captcha