IQNA

12:33 - July 04, 2026
Habari ID: 3482439

Bendera na nara za Palestina zatawala Kombe la Dunia la 2026 huku mashabiki wakionyesha Mshikamano

IQNA – Mashindano ya Kombe la Dunia la 2026 yanafanyika kote Amerika Kaskazini, lakini “sauti” kuu ya michuano hiyo inayoimbwa bila shaka ni ile ya kuunga mkono Palestina.

Mashabiki wa mataifa yanayoshiriki katika Kombe la Dunia la FIFA la 2026, linaloandaliwa kwa pamoja na Marekani, Kanada, na Mexico, wamekuwa wakionyesha uungaji mkono wao kwa Palestina katika viwanja vya umma kabla ya mechi na ndani ya viwanja wakati wa michezo.

Katika kipindi chote cha Kombe la Dunia, mashabiki wamekuwa wakipeperusha bendera za Palestina, wakidai uhuru kwa ajili ya Palestina, na kupinga vikali mauaji ya kimbari yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Mataifa mengi yanayoshiriki michuano hiyo pia yameunga mkono wito wa kimataifa kutoka kwa mashabiki wa “kuionyesha Israel kadi nyekundu” kutokana na jinai za mauaji ya kimbari.

Wakati timu ya taifa ya Uturuki ilipoichapa Marekani mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho ya Kundi D, bendera ya Palestina iliyokuwa ikipeperushwa uwanjani nyuma ya goli iliendelea kuonekana kwa muda wote wa mechi hiyo na shabiki wa Kituruki.

Katika mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Ujerumani na Paraguay, familia ya watu watatu, ikijumuisha mtoto, ilionekana ikipeperusha bendera za Palestina. Shabiki mmoja wa Palestina, ambaye pia ana uraia wa Marekani, aliambia mwandishi wa habari wa Anadolu, “Sisi ni raia wa Marekani wenye asili ya Palestina. Tunasherehekea kwa ajili ya Palestina katika Kombe hili lote la Dunia. Hawatatuacha kamwe. Palestina na iwe huru!”

Mashabiki wa Morocco, walioenda sare ya 1-1 na Brazil katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi C, walionyesha mshikamano wao kwa Palestina katika viwanja vya New York kabla ya mchezo, na katika majukwaa ya watazamaji wakati wa mechi. Katika Uwanja wa New York New Jersey, ambao pia utakuwa mwenyeji wa fainali, mashabiki wa Morocco walioonyesha uungaji mkono wao kwa Palestina kila walipopata nafasi, walibeba bendera ya Palestina kwenye majukwaa nyuma ya goli.

Kabla ya mechi hiyo, walikusanyika katika eneo la Times Square jijini New York, wakipeperusha bendera za Palestina na kuimba kauli mbiu kama “Palestina na iwe huru!” Mashabiki wa Morocco pia walionyesha mshikamano wao wakati wa mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Uholanzi.

Bendera za Palestina pia zilipopeperushwa wakati wa mechi kati ya Bosnia na Herzegovina na Uswizi huko Los Angeles. Wabosnia, ambao walipitia mauaji ya kimbari kati ya mwaka 1991 na 1995, hawakumsahau Palestina, watu wanaoshiriki hatima kama yao. Mashabiki wao walibeba bango lililoandikwa: “Uungaji mkono kwa Palestina kutoka Sarajevo.”

Wakati wa mechi kati ya Bosnia na Herzegovina na Qatar, shabiki mmoja alibeba bendera za Palestina uwanjani. Shabiki wa Qatar, akiwa amevalia kofia ya kitamaduni ya Palestina (keffiyeh) na kupaka rangi usoni, alidhihirisha wazi msimamo wake wa kuunga mkono Palestina.

Mashabiki wa Ufaransa, ilioishinda Senegal 3-1 katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi I, walipeperusha bendera ya Palestina ndani ya uwanja. Wakati wa mechi hiyo katika Uwanja wa New York New Jersey, ambapo mabingwa wa 2018 na washindi wa pili wa 2022 Ufaransa walipokutana na Senegal, shabiki wa Ufaransa alionekana akiwa ameshikilia bendera ya Palestina kabla ya mchezo kuanza.

Kabla ya mechi ya Brazil dhidi ya Japan katika hatua ya 16 bora, mashabiki wa “Samba Boys” waliandamana kuelekea uwanjani kwa wingi, na mmoja wa mashabiki katika kundi hilo alibeba bendera ya Palestina.

Nje ya uwanja wa Seattle ulioandaa mechi ya Misri na Iran, mwanamke aliyevaa vazi la “Sanamu ya Uhuru” alidai “uhuru” kwa ajili ya Palestina na Lebanon huku akionyesha bendera za mataifa hayo mawili. Bendera za Palestina pia zilichukuliwa uwanjani wakati wa mechi hiyo kati ya mataifa hayo mawili yenye idadi kubwa ya Waislamu.

Mataifa mengi yanayoshiriki michuano hiyo yameelezea uungaji mkono wao kwa Palestina na upinzani dhidi ya mauaji ya kimbari. Mataifa ya Ulaya yanayojulikana kwa uungaji mkono wao wa wazi kwa Palestina, kama vile Uhispania, Scotland, Uturuki, na Bosnia na Herzegovina, pamoja na mataifa ya Afrika kama Morocco, Senegal, Algeria, Misri, na Iran kutoka Asia, yameshiriki katika michuano hii.

Vilabu vya soka kutoka nchi mbalimbali vinaunga mkono wito wa mashabiki katika jamii ya soka duniani wa “kuionyesha Israel kadi nyekundu.” Katika kipindi cha mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel, ambayo yamesababisha pia Gaza kukumbwa na njaa, zaidi ya wanariadha 1,000, wengi wao wakiwa wanasoka, wameuawa, na karibu vituo 300 vya michezo vimeharibiwa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Wakati nchi na timu kote ulimwenguni zikidai kuwa Israel ipigwe marufuku kushiriki mashindano yoyote ya michezo, wanariadha nyota kutoka mataifa mengi pia wanapaza sauti zao kupinga mauaji ya kimbari ya Israel.

captcha