“Hii ni tahadhari kwa wanadamu kwamba kutoadhibiwa kwa wahalifu, na kukosekana kwa uwajibikaji kamwe havikubaliki kuwa ndiyo kanuni mpya ya kimataifa,” alisema Mohamad Azmi Abdul Hamid katika taarifa yake, akilaani vikali mauaji ya kigaidi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei yaliyotekelezwa na Marekani na utawala wa Kizayuni.
Taarifa hiyo imesema:
Mazishi ya Kiongozi Muadhamu Shahidi wa Iran, Ayatullah Syed Ali Khamenei, ni zaidi ya tukio la kuomboleza kiongozi wa kitaifa. Ni ukumbusho mzito wa matokeo mabaya ya ugaidi wa kiserikali, mauaji ya kisiasa, na kuhalalishwa kwa hatari kwa tabia ya kutoadhibiwa katika masuala ya kimataifa.
Mauaji yaliyotekelezwa kupitia uchokozi wa Marekani na Israel ni sura nyingine katika mlolongo mrefu wa ukiukaji wa sheria za kimataifa, uhuru wa kitaifa, na utukufu wa uhai wa binadamu. Vitendo kama hivi haviwezi kuhalalishwa chini ya fundisho lolote la kujilinda au usalama wa taifa.
Jumuiya ya kimataifa lazima ikatae majaribio ya kuhalalisha mauaji kama nyenzo ya sera za kigeni. Pale mataifa yenye nguvu yanapoweza kuondoa viongozi wa kisiasa na kidini bila kuwajibika, mfumo mzima wa sheria za kimataifa unadhoofika. Kunyamaza kimya mbele ya uhalifu huu ni sawa na kushiriki katika uhalifu huo.
Hadhira ya mazishi haya inadhihirisha kwamba ingawa viongozi wanaweza kuuawa shahidi, fikra na malengo yao hayawezi kufutwa kwa ghasia. Historia inatuonyesha mara kwa mara kwamba dhuluma mara nyingi huimarisha azma ya watu katika kutetea haki, utu, na uhuru wa kitaifa.
MAPIM inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, serikali, mashirika ya kiraia, na watetezi wa haki za binadamu kudai:
1. Uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu mauaji hayo na wahusika wote wanaohusika.
2. Uwajibikaji kamili kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu.
3. Kukomeshwa kwa sera ya mauaji ya kiholela (extrajudicial killings) na mauaji ya kisiasa.
4. Utekelezaji sawa wa sheria za kimataifa bila vigezo maradufu.
5. Hatua madhubuti za kuzuia mmomonyoko zaidi wa utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria.
Umma wa Kiislamu na watu wote wenye dhamiri lazima wabaki imara katika kupinga dhuluma kokote ilipo. Haki ya kuchagua (kuchagua nani wa kumtetea) ni dhuluma yenyewe. Uwajibikaji wa kuchagua ni sawa na kutoadhibiwa. Ikiwa ulimwengu utakubali mauaji ya kisiasa kuwa jambo la kawaida, hakuna taifa wala kiongozi yeyote atakayekuwa salama dhidi ya uchokozi haramu.
Mazishi ya Kiongozi Muadhamu Shahidi, kwa hivyo, yanatoa ujumbe unaovuka mipaka ya Iran. Ni onyo kwa wanadamu kwamba kushirikiana na wahalifu, kutoadhibiwa kwa wahalifu, na kukosekana kwa uwajibikaji kamwe havikubaliki kuwa ndiyo kanuni mpya ya kimataifa.
Mohd Azmi Abdul Hamid
Rais
Baraza la Ushauri la Mashirika ya Kiislamu ya Malaysia (MAPIM)
3498072