IQNA

Mwanafikra wa Uswisi atunukiwa zawadi ya 'kukurubisha pamoja Uislamu na Ukristo'

11:07 - December 06, 2008
Habari ID: 1716088
Kituo cha Kukurubisha Pamoja Uislamu na Ukristo cha Mwanamfalme al-Walid bin Talal kimempa zawadi ya 'kukurubisha pamoja Uislamu na Ukristo' mwanafikra wa Uswisi Hans Kung.
Msomi huyo ni mhadhiri wa masuala ya kidini nchini Marekani. Sababu ya msomi huyo kupewa zawadi hiyo imetajwa kuwa ni juhudi zake kubwa katika kufanya utafiti wa masuala ya Kiislamu na hatimaye kuandika kitabu kiitwacho, 'Uislamu, historia, hivi sasa na baadaye' katika Chuo Kikuu cha George Town nchini Marekani. Sherehe za kutunukiwa zawadi iliyotajwa kwa msomi huyo zilihudhuriwa na idadi kubwa ya shakhsia wa kielimu na wa vyuo vikuu. Kitabu kilichotajwa kimekuwa na athari kubwa nzuri katika ulimwengu wa Kiislamu, na ndio maana mwandishi wake akatunukiwa zawadi hiyo.330052
captcha