IQNA

Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu na Qur’ani mjini New York

11:17 - December 06, 2008
Habari ID: 1716227
Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu na Qur’ani Tukufu yanatazamiwa kuanza tarehe 19 mwezi huu wa Disemba hadi 9 Januari katika jumba la makumbusho la Asia Society mjini New York, Marekani.
Kazi zaidi ya 160 za kaligrafia au sanaa ya kuandika vizuri kurasa za Qur’ani na maandiko mengine ya Kiislamu zitaonyeshwa katika maonyesho hayo yanayofanyika kwa ushirikiano wa jumba la makumbusho la sanaa la Huston na jumba la makumbusho la Chuo Kikuu cha Harvard. Kazi hizo zinahifanyiwa katika majumba hayo ya makumbusho.
Vilevile kazi za kisanii za waandishi Waislamu wa kuanzia karne ya 17 hadi 19 kutoka nchi za Iran, Uturuki na India zitaonyeshwa katika maonyesho hayo. 330059


captcha