Kundi moja la wanazuoni wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri limetoa taarifa likisema kuwa, kitendo cha Muhammad Sayyid Tantawi, mkuu wa chuo hicho cha kumpa mkono Shimon Peres, Rais katili wa utawala ghasibu wa Israel walipokutana hivi karibuni huko New York nchini Marekani ni hatua aliyoichukua kama mtu binafsi na kwamba inakinzana na msimamo rasmi wa chuo hicho kuhusiana na utawala huo.
Katika taarifa hiyo, maulamaa hao wamesema kuwa ikiwa taasisi muhimu na kubwa zaidi ya kidini katika ulimwengu wa Kiislamu, chuo hicho kinapinga vikali juhudi za kuboreshwa uhusiano wa ulimwengu wa Kiislamu na utawala huo ghasibu. Taarifa hiyo inasema kuwa katika hali ambayo Waislamu wa Palestina wa Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na mzingiro wa kidhulma wa utawala wa Israel na jinai za utawala huo kukabiliwa na upinzani mkubwa wa kimataifa, ni jambo lisilofaa kwa mkuu wa al-Az'har kuzungumzia suala la kuboresha uhusiano wa nchi za Kiislamu na utawala huo. Katika upande wa pili, wanazuoni wengine wa chuo hicho wamechukua msimamo wa kihafidhina zaidi na kusema kuwa hatua hiyo ya Tantawi kumpa mkono katili Peres ni ya kisiasa na wala haihusiani na masuala ya al-Azhar. 330780