IQNA

Sisitizo la mwakilishi wa Ayatullah Sistani juu ya kutekelezwa hati ya Makka

11:53 - December 07, 2008
Habari ID: 1716773
Abdulmahdi al-Karbalai, mwakilishi wa Ayatullah Sistani mjini Karbala amesisitiza umuhimu wa kutekelezwa makubaliano na hati ya mji mtakatifu wa Makka ambayo ilipitishwa mwaka 2006.
Akiashiri kikao kilichofanyika tarehe 4 Disemba kati ya wanazuoni wa Kishia na Kisunni mjini Makka, Abdulmahdi amesema kuwa kikao hicho kilisisitiza umuhimu wa kutekelezwa hati hiyo ya mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja miongoni mwa wanazuoni wa madhehebu mbili hizo na kusimamisha umwagaji damu ya Waislamu. Amesema kuwa kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na wanazuoni wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali kilisisitiza udharura wa kuimarishwa umoja miongoni mwa Waislamu, kujiepusha na fitina na mfarakano pamoja na migawanyiko ya kikabila na kimadhehebu. Abdulmahdi al-Karbalai amesema, kufanyika kwa vikao kama hivyo vya kuhifadhi umoja wa Waislamu na kukabiliana na taasubi za kimadhehebu kuna umuhimu mkubwa na kusisitiza umuhimu wa kuundwa kamati za kufuatilia maamuzi ya vikao kama hivyo. Amemaliza kwa kusema, kuenezwa kwa utamaduni wa mazungumzo na usamehevu ni jambo linalosaidia sana katika kuleta amani ya kudumu katika ulimwengu wa Kiislamu. 330432
captcha