Mwandishi wa IQNA amesema, katika kitabu hicho chenye kurasa 86 Ustadh Shalbi amefanya jitihada za kufafanua mafundisho ya dini ya Kiislamu kwa Wasiokuwa Waislamu.
Sehemu moja ya kitabu cha Uislamu; Dini ya Maisha, Shalbi ambaye amehitimu masomo ya teolojia ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri amebainisha misingi ya ibada ya Hija, itikadi za Kiislamu na desturi za dini hiyo tukufu. 330671