Shirika rasmi la Habari la Saudi Arabia (SPA) limemnukuu Naibu Mwenyekiti wa Idara ya Masuala ya Masjidun Nabii Muhammad bin Nasir al Khaziim akisema kuwa shughuli hiyo ya kubadilisha pazia la al Kaaba ilihudhuriwa na wawakilishi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu na kwamba pazia hilo lilitengenezwa katika karakana ya kushona pazia la al Kaaba mjini Makka. Pazia hilo limeshonwa kwa kutumia kitambaa cha hariri na dhahabu halisi.
Muhammad bin Nasir amesema, juu ya mkanda uliaotumiwa kufunga pazia hilo la Nyumba ya Mwenyezi Mungu kumeandikwa aya za Qur'ani Tukufu. 331046