Katika ujumbe wake huo, Rais Ahmadinejad ametoa salamu za pongezi, heri na fanaka kwa serikali na matiafa yote ya Waislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Adh'ha.
Rais wa Iran ameitathmini sikukuu ya Idul Adh'ha kuwa dhihirisho la ibada kwa Mwenyezi Mungu.
Rais Ahmadinejad amemuomba Mwenyezi Mungu ayape mataifa yote ya Kiislamu mafanikio, heshima na furaha.
Aidha ametoa wito kwa Waislamu na nchi za Kiislamu kote duniani kudumisha umoja na mshikamano.
Wakati huo huo Rais Ahmadinejad amemtumia ujumbe Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Prof. Ekmeleddin Ihsanoglu na kumpongeza kwa munasaba wa kuwadia sikukuu ya Idul Adh'ha. 331657