IQNA

Bunge la Misri kujadili njia za kukabiliana na tuhuma dhidi ya Uislamu.

12:14 - December 09, 2008
Habari ID: 1717462
Kamisheni ya Masuala ya Dini ya Bunge la Misri imeazimia kuchunguza njia za kukabiliana na tuhuma chafu zinazotolewa na makundi ya kufurutu mipaka ya nchi za Magharibi kwa kuchapisha kitabu kitakachozungumzia maisha ya Nabii Muhammad (saw).
Bunge la Misri linatarajiwa kukutana kesho kujadili njia za kukabiliana na matusi na vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu hususan Mtume Muhammad (saw). Kikao hicho kitahudhuriwa pia na Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu Mahmoud Hamdi Zaqzuq, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Misri na wahadhiri wa vyuo vikuu.
Washiriki katika kikao hicho watabadilishana mawazo kuhusu kitabu hicho cha maisha ya Nabii Muhammad na lugha nyingine ambazo zitatumiwa kukitarjumu.
Khalid Zardaq ambaye ni mwanachama wa Kamisheni ya Masuala ya Dini ya bunge la Misri amesema kuwa uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho unahitaji kupasishwa na bunge na baadaye jumuiya na taasisi mbalimbali za Kiislamu zinaweza kushiriki katika kukusanya maudhui zake. Vilevile waandishi na wanazuoni wa Kiislamu wanaweza kutoa mapendekezo yao kuhusu njia za kujibu mashambulizi na hujuma za Wamagharibi dhidi ya Mtume Muhammad (saw). 331543
captcha