IQNA

Mkataba wa usalama wa Baghdad-Washington hauna faida yoyote kwa Wairaki

12:54 - December 10, 2008
Habari ID: 1717632
Ibrahim Jaafari, Mkuu wa Chama cha Marekebisho ya Kitaifa ya Iraq amesema kuwa kutiwa saini mkataba wa usalama wa serikali za Baghdad na Washington kutatoa fursa kwa Wamarekani kuidhibiti kisiasa Iraq na kuongeza kuwa, mkataba huo hauna faida yoyote kwa taifa la Iraq.
Kwa mujibu wa tovuti ya www.eslahiraq.com, Ibrahim Jaafari amesema kuwa mkataba huo unazuia kivitendo kupatika kwa demokrasia katika jamii ya Iraq na kuongeza kuwa, chama chake kinaupinga vikali. Amesisitiza kuwa mkataba huo utakuwa na madhara makubwa kwa Wairaki na kuwa utatoa mwanya wa kuingilia kisiasa Marekani masuala ya ndani ya Iraq. Mwishoni amesisitiza umuhimu wa kufanyika uchaguzi wa mabaraza ya miji nchini humo katika wakati uliopangwa na kwamba, uchaguzi huo utaimarisha uthabiti wa kisiasa wa nchi hiyo. Chama hicho cha Jaafari kilitoa taarifa siku mbili tu baada ya kupitishwa mkataba huo katika bunge la Iraq, kikipinga utiwaji saini na utekelezwaji wa mkataba huo nchini Iraq, kabla ya wananchi kufahamishwa maana na malengo yake halisi.
Ni muhimu kuashiria hapa kwamba, wanazuoni mashuhuri wa kidini katika ulimwengu wa Kiislamu na hasa wa Iraq wakiwemo Ayatullah Ali Sistani, Ayatullah Sayyid Kadhimi Hairi, Ayatullah Muahammd Ya'qubi na Ayatullah Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah wa Lebanon walimtahadharisha Wazir Mkuu wa Iraq Nur al-Maliki wakimtaka asitie saini mkataba huo hadi wakati wa kudhaminiwa kikamilif maslahi ya wananchi pamoja na kujitawala kwa nchi hiyo. Katika upande wa pili, Muqtada Swadr, mwanazuoni mwingine wa Iraq alitangaza siku tatu za maombolezo ili kulalamikia utiwaji saini mkataba huo baada ya kupitishwa na bunge la nchi hiyo.331762
captcha