Jumba la makumbusho la “Utamaduni wa Kiislamu” litafunguliwa hivi karibuni katika eneo la kihistoria la Intramuros katika mji mkuu wa Ufilipino, Manila kwa shabaha ya kudhihirisha utajiri wa ustaarabu na utamaduni wa Kiislamu.
Mbunge wa Baraza la Seneti la Ufilipino Richard Gordon amesema kuwa mpango wa kuasisi jumba la makumbusho la Utamaduni wa Kiislamu nchini humo ni sehemu ya juhudi za kuzidisha maarifa ya wananchi kuhusu taathira ya utamaduni wa Kiislamu kwa watu wa nchi hiyo. Amesema kuwa ujenzi wa jumba hilo la makumbusho utakuwa na taathira nzuri katika kuonyesha mchango wa Waislamu katika historia ya Ufilipino na kueneza amani kati ya Waislamu na Wakristo wa nchi hiyo.
Gordon amezitaka nchi za Kiislamu kutoa misaada ya kifedha kwa ajili ya ujenzi wa jumba la makumbusho la Utamaduni wa Kiislamu.
Uislamu uliingia katika visiwa vya Ufilipino miaka mia mbili iliyopita na kwa sasa karibu Waislamu milioni nne wanaishi nchini humo. 332182