Mwanachama wa baraza la mji wa Leidschendam-Voorburg wa Uholanzi Ihsan Jami jana alionyesha filamu hiyo, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na jumuiya za Kiislamu nchini humo.
Taarifa ya jumuiya za Kiislamu za Uholanzi imesema kuwa filamu ya Mahojiano na Muhammad haina maana na imewataka Waislamu kutofanya maandamano ya ghasia na fujo ambayo yanaweza kutumiwa vibaya na makundi yenye misimamo mikali.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi amekutana na Mabalozi wa nchi kadhaa za Kiislamu akieleza wasiwasi wake kuhusu jibu la Waislamu dhidi ya filamu hiyo inayovunjia heshima matukufu ya dini yao.
Katika filamu hiyo fupi, mchezaji aliyepewa nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu anajibu maswali kadhaa kuhusu wanawake, Mayahudi na uhuru wa mtu kuacha dini ya Kiislamu. 332661