Tovuti ya mwanazuoni huyo imevitaka vyombo vyote vya habari vya nchi hiyo vifanye juhudi za kuwa angalifu katika kuakisi kwa usawa na usahihi habari na matamshi yanayolewa na wanazuoni wa Iraq kuhusiana na masuala mbalimbali ya nchi hiyo. Amesisitiza muhimu wa nafasi ya wanawake na tabaka la vijana wa Iraq katika kustawisha uchumi wa nchi na kutaka kuandaliwa uwanja unaofaa kwa ajili ya kuwashirikisha katika miradi na shughuli mbalimbali za ustawi wa nchi hiyo.
Imam huyo wa mji mtakatifu wa Najaf amemaliza matamshi yake kwa kuwataka Wairaqi washiriki kwa wingi katika uchaguzi ujao wa mabaraza ya miji akisema kuwa, uchaguzi huo utakuwa moja ya hatua muhimu za kuleta maendeleo nchini humo. 333026