IQNA

Kugunduliwa kwa sarafu za kale za Kiislamu nchini Norway

11:37 - December 14, 2008
Habari ID: 1718910
Mkurugenzi wa jumba la makumbusho la taifa la mji wa Oslo nchini Norway Cristoph Kilger amesema kuwa safaru za kale za Kiislamu za kipindi cha karne ya nane Miladia zimegunduliwa nchini humo.
Cristoph Kilger amesema: Wataalamu wa vitu vya kale wanaamini kwamba sarafu hizo za kihistoria za Kiislamu ziliingizwa katika eneo la Scandinavia na wafanyabiashara wa Caucasia. Amesema: Muhuri wa Khalifa wa Baghdad katika zama za utawala wa Bani Abbas unaonekana juu ya sarafu hizo na kwamba zilitengenezwa mwaka 750 Miladia.
Mkurugenzi wa jumba la makumbusho la taifa la Oslo amesema kuwa, wataalamu wa mambo ya kale wamesisitiza katika utafiti wao kwamba nchi za Kiislamu zimekuwa na uhusiano mzuri na nchi za Scandinavia katika vipindi mbalimbali vya historia.
Eneo la Scandinavia linajumuisha nchi za Ulaya kaskazini za Sweden, Norway, Finland, Iceland na Denmark. 333062
captcha