Kongamano hilo limefanyika kwa shabaha ya kubainisha nafasi ya Uimamu na uongozi katika Uislamu na katika mtazamo wa Imam Ali (as).
Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Zambia Muhammad Asadi Muwahhid amesema kuwa moja ya malengo ya kongamano hilo ni kuwafafanulia Waislamu na jamii ya Wakristo ya Zambia matukufu na fikra za Imam Ali bin Abi Twalib. Ameongeza kuwa Sheikh Ibrahim Juma alihutubia kongamano hilo akizungumzia nafasi ya Uimamu na uongozi wa umma wa Kiislamu katika Qur’ani.
Kitabu cha al Ghadir kilichoandikwa na Allamah Amini akifafanua tukio la Ghadr ambapo Ali bin Abi Twalib alitambulishwa na Mtume Muhammad kuwa khalifa na kiongozi wa Waislamu baada yake, kiliarifishwa katika Kongamano hilo.
Sambamba na kongamano hilo kulikuwepo maonyesho ya vitabu vya Kiislamu, sayansi ya Qur’ani na CD za Qur’ani ambayo yamefanyika katika maktaba kuu ya Chuo Kikuu cha Zambia. 334375