IQNA

Waislamu wa Iraq waandamana wakitaka kuachiwa huru Muntadhir Zaydi

11:17 - December 20, 2008
Habari ID: 1720548
Waislamu wa maeneo mbalimbali ya Iraq wameandamana wakitaka kuachiwa huru mwandishi wa habari aliyemfedhehesha Rais George Bush wa Marekani kwa kumrushia viatu.
Waandamanaji hao walitetea kitendo cha mwandishi huyo wa habari na kutangaza upinzani wao dhidi ya kutiwa kwake korokoroni.
Habari zinasema kuwa mawakili zaidi ya mia mbili wakiwemo wanasheria wa Marekani wamesema, wako tayari kumtetea Zaydi katika mahakama ya Iraq.
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya mpira wa miguu wa Iraq Adnan Hamd amempongeza Muntadhir Zaydi kwa kumfurumushia Bush viatu katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Baghdad na akasema kwamba yuko tayari kununua viatu hivyo kwa dola laki moja za Kimarekani.
Adnan Hamd amesema: Viatu alivyorushiwa George Bush na mwandishi huyo wa habari ni viatu ya heshima na utukufu wa Wairaqi na kwamba kitendo hicho kimerejesha hadhi iliyopotea ya wananchi wa Iraq.
Tarehe 14 mwezi huu wa Disemba, mwandishi wa habari wa kanali ya televisheni ya al Baghdadiyya ya Iraq Muntadhir Zaydi aliyeshiriki katika mkutano wa waandishi habari wa Rais George Bush na Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki alimpopoa kwa viatu kiongozi huyo wa Marekani huku akimwita mbwa.
Rais Bush amekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kustaajabisha mno katika kipindi chote cha utawala wake huko Marekani. 334916

captcha